EQWIP HUBs, Ni sehemu rafiki kwa vijana kujipatia mafunzo, ujuzi, rasilimali na msaada utakaowawezesha kuanzisha shughuli zao za kiuchumi, kutafuta kazi pamoja na kuwapatia uzoefu wa uongozi na matumizi ya technologia. Mafunzo haya yanatolewa katika Miji mitatu, Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar. Nyote mnakaribishwa na mafunzo yatolewa bila ya malipo yoyote. Wanafunzi wenye mtiririko wa kijasiriamali watakuwa na nafasi ya kuomba katika Mfuko wa uwezeshaji kwa Vijana. Mfuko huu unayapa mawazo bora ya biashara fedha ili vijana kuanza biashara zao. Mafunzo ya tertiary hupatikana nje ya darasa. Mafunzo haya ukamilisha mafunzo ya awali. Mafunzo ya awali (Moduli) 1. Maendeleo ya mtu binafsi - 2. Mawasiliano baina ya watu - 3. Uongozi na ushirikiano - 4. Ukomavu wa kifedha - 5. Utangulizi wa ujasiriamali - 6. Uelewa wa Kidijitali Ajira 1. Kanuni za utumishi na Utendaji Bora - 2. Usalama na Afya kazini - 3. Haki na Wajibu Au Ujasiriamali 1. Utagulizi wa ujasiriamali - 2. Sifa za ujasiriamali - 3. Kutafuta wazo zuri la biashara - 4. Masoko - 5. Shughuli, Rasilimali, Washirika, wateja na Mapato - 6. Masuala ya Fedha - 7. Kuendesha Biashara